Kilimo cha Vitunguu
Kitunguu ni zao lenye uhitaji mkubwa duniani. Kila familia inahitaji kitunguu kwenye maandalizi ya mlo, hii inamaanisha mkulima wa kitunguu ana soko la uhakika. Kitunguu hubadilisha uchumi wa mkulima, kutokana na faida kubwa anayoweza kupata ndani ya msimu mmoja.